Jumatano, 15 Juni 2016

BORN TO DIE, RIWAYA INAYOZUNGUMZIA MATATIZO YA AFRIKA. KILA SIKU SAA 8 KAMILI MCHANA



RIWAYA: Born To Die
NA:Frank Masai

SEHEMU YA 1.

“What is your name? (Jina lako nani)?”
“I don’t know. (Sijui)”.
“Pu pu pu”.Zilisikika sauti hizo kwenye chumba kimoja kidogo kilichokuwa na watu watano.
Sauti hizo zilikuwa ni sauti za kipigo kumwendea yule aliyekuwa anaulizwa maswali.

Jamaa hao watano,mmoja ambaye ndiye alionekana mkuu, alikuwa anauliza maswali,wengine wawili wamemshikilia kwa nguvu jamaa mwingine aliyekuwa anaulizwa maswali,huku wamemkunja mikono kwa nyuma na kufanya kifua na tumbo lake kubetuka vizuri kwa mbele.Kitu kilichompa yule jamaa wa tano kumshushia kipigo cha nguvu pale alipokaidi kujibu maswali yao.

“I asking you again.If you don’t answer, we will kill you (Nakuuliza tena. Kama usipojibu, tunakuua)”.Yule mkuu wao ambaye alivalia mavazi ya kijeshi, tena yale yenye nyota nyingi mabegani na kwenye mifuko ya shati lake.Alimpa onyo jamaa yule aliyekuwa anapewa kipigo huku akiwa amechakaa uso kwa damu pamoja na kuvimba vibaya mno.
Alishapoteza matumaini ya kuishi kwani mwili wake ulikuwa umelegea kiasi kwamba alikuwa anawapa uzito wale waliokuwa wamemshikilia.

“What is your name (Jina lako nani)?”Jamaa aliulizwa swali.
“I don’t know Sir (Sijui Mzee)”.Alijibu yule jamaa kwa sauti ya chini iliyokuwa imeishiwa nguvu kabisa.
Yule mpigaji alivyoona hivyo, alinyanyua ngumi yake tayari kuendelea kuishindilia mwilini mwa yule jamaa.

“Stop (Acha)”.Yule mkuu alimkataza mpigaji.

“You are so rude, boy.That is good (Unaonekana mkorofi kijana.Safi sana)”.Mkuu yule aliongea huku akizunguka zunguka kile chumba kwa tambo.

“Release him.(Muachieni)”.Aliwaambia wale jamaa waliokuwa wamemshika na wao wakatii amri kwa kumwachia yule mtuhumiwa wao.

“You all, go outside (Ninyi nyote, nendeni nje)”.Aliendelea kuwaamuru wale jamaa waliokuwamo mle ndani, nao wakatoka na kumuacha yule jamaa kalala chini akigugumia kwa maumivu.

“Okey.Now we are alone.You have to tell me the truth.(Sawa.Sasa tupo peke yetu.Unatakiwa kuniambia ukweli ”.Aliongea mkuu yule huku akichutama karibu na pale alipokuwa amelala yule jamaa.

“I have nothing to tell you (Sina cha kukuambia)”.Alijibu jamaa yule kwa sauti ya ukakamavu lakini iliyojaa maumivu.

“That’s bad boy. So damn bad. (Hiyo mbaya kijana.Tena mbaya sana)”.Aliongea yule mkuu huku akisimama toka eneo lile na kwenda kwenye jiko moja la umeme ambapo alikuwa ametenga birika la maji.

Akachukua birika lile na kwenda nalo kwenye meza iliyokuwamo mle, kisha akamimina maji yale kwenye kikombe na kuchukua kahawa kiasi kwenye kijiko na kuchanganya kwenye maji yaliyo kwenye kikombe.

Alivuta kiti kwa nyuma na kukikalia, kisha akafunua sahani moja iliyokuwepo mezani pale na kuchukua chapati moja.
Aliikunja chapati ile na kuanza kuila huku akishushia kwa kahawa aliyoichanganya muda mfupi uliopita.

Katikati ya ulaji wake, alimtupia jicho yule jamaa aliyekuwa amelala pale chini.Alimwona jinsi anavyomwangalia alavyo, naye akatumia udhaifu huo kuongea naye.

“Are you hungry? (Una njaa?)”.Alimuuliza yule jamaa huku bado anatafuna kipande cha chapati alichokuwa kabwia mdomoni.

“Come on. Let’s eat. (Njoo. Njoo tule)”Aliongea yule mkuu na kunyanyuka pale kitini na kwenda kwenye kabati moja kuu-kuu la vyombo na kuchukua kikombe kimoja cha plastiki na kwenda nacho mezani.

“Don’t you want it? (Hautaki?)”Alimuuliza yule jamaa aliyekuwa amelala pale chini baada ya kumwona hajishughurishi kuitikia karibu yake.

Jamaa yule aliyekuwa chini alianza kuinuka pale alipokuwa na moja kwa moja akaelekea kuungana na yule mkuu kwenye meza ile.

“That is my man.(Huyo ndiye mtu wangu)”.Alimsifia jamaa alipokuwa ananyanyuka huku yeye akimimina maji kwenye kile kikombe alichokuja nacho mara ya pili.

Jamaa naye alivuta kiti kiuchovu na kukaa huku akimuelekea yule mwenyeji uso. Akapewa kahawa kwenye kikombe kile na kusogezewa sahani ya chapati ili ajilie.

Alikula kwa taratibu na kistaarabu kuliko alivyotegemea yule mkuu aliyekuwa anamuangalia kwa macho ya kumdadisi yule jamaa ambaye alikuwa kifua wazi na chini kavaa kombati ya jeshi yenye mabaka ya kijani.

“So.Tell me soldier boy. Who are you and who sent you here (Niambie kijana. Wewe ni nani na nani kakutuma hapa?)”.Yule mkuu alimuuliza huku akiweka miguu yake mezani.

“I am nobody and nobody sent me here. (Mi si kitu na hakuna aliyenituma hapa)”.Jamaa alijibu na kisha aliinamia kahawa yake na kuendelea kuinywa.

“You act like a taugh guy.Am I right boy? (Unajifanya kijana mgumu sana.Nadanganya kijana?)”.Mkuu alimuuliza huku bado miguu yake ikiwa pale mezani anaitikisa tikisa kwa mbwembwe.

“No. I just answer your questions. But if you like me to be a tough guy,I will. But don’t blame me. (Hapana. Najibu maswali yako. Lakini kama unapenda niwe mgumu, nitakuwa. Lakini usinilaumu)”.Jamaa alijibu huku anasogeza kikombe cha kahawa na sahani mbele kumuelekea yule mkuu.

“You never answer my questions boy. And don’t try me to make you like before. (Hujanijibu maswali yangu kijana. Na usinijaribu nikufanye kama hapo mwanzo)”.Mkuu aliongea huku macho yake kamkazia yule jamaa ambaye alikuwa hataki kujitambulisha.
Jamaa alikaa kimya huku naye macho yake anamuangalia yule mkuu ambaye umri kiasi fulani ulikuwa umeenda lakini alikuwa bado mkakamavu.

Akiwa ndani ya mavazi yake ya nyota, mkuu yule alishusha miguu yake juu ya meza na kusogea mbele zaidi na kumkingia uso yule jamaa.

“Umetumwa na Urusi? Cuba au Korea?”Mkuu yule alimuuliza kwa lugha ileile ya kiingereza.
Jamaa akacheka kwa dharau kisha akamuangalia yule mkuu na kuhisi kama anapoteza dira.

“Kwa nini ziwe nchi hizo na siyo zile mnazowatengenezea silaha za maangamizi na kuwapa ili muone kama zinafanya kazi ipasavyo? Kwa nini zisiwe zile nchi ambazo mnazichukulia malighafi zake na kujilimbikizia nyie? Kwa nini zisiwe zile nchi ambazo kila siku zinalia na njaa huku zikipoteza watoto wake kwa waume kwa sababu ya vita ambavyo nyie ndio wachonganishi? Kwa nini zisiwe nchi mnazozuga mnatandaza demokrasia, kumbe mnatandaza vita? Kwa nini zisiwe hizi nchi mnazozitupia magonjwa kila kukicha?
 Kwa nini zisiwe nchi hizo na badala yake zikawa nchi ambazo zinatetea msifanye maasi yenu?” Aliongea yule jamaa kwa sauti ya chini iliyoanza kupata ahueni baada ya maumivu kupoa kiasi. Aliongea kwa hasira na msisitizo ndani yake.

“Kwa hiyo umetokea Afrika”.Aliongea yule mkuu huku akirudisha mgongo wake kwenye kiti na kuweka miguu yake mezani tena na mikono yake akiipitisha shingoni na kuja kukutana nyuma ya kisogo chake.

“Well, well.Umetoka Afrika. Niambie sasa. Umetoka Kongo, Kameruni au Naijeria.Au labda umetoka Niger au Sudan”.Alizidi kubwabwaja yule mkuu.

“Nimetokea Afrika.Siwakilishi nchi wala Taifa”.Jamaa alijibu kwa nyodo na kwa kujiamini.

“Okey. Sasa ni muda wa kuwa siriazi. Nauliza na unajibu ipasavyo, sawa?”Mkuu yule alikuja juu sasa na kumtaka yule jamaa mwenye ngozi nyeusi awe siriazi.

“Ni wewe ndiye haupo siriazi. Nipo siriazi hata kwenye kula.Ni vema uwahi kusema ulichokusudia kuliko kuniacha na kwa kuendelea kuniuliza maswali. Sitataja jina langu,wala hutojua nipo hapa kwa ajili gani”.Jamaa aliweka msisitizo kwa akifanyacho.

“Utakufa kijana”.Mkuu aliongea huku akiendelea kumwangalia kwa uangalifu yule jamaa.

“I was BORN TO DIE”. Jamaa alimjibu mkuu na kumuacha mkuu akiwa kinywa wazi bila kusema neno.
Maneno yale yalidhihirisha kuwa jamaa haogopi wala kuhofia jambo lolote litakalokuja kumtokea mbeleni.

“Nakuuliza mara ya mwisho. Wewe ni nani na nani kakutuma”.Mkuu aliuliza kwa hasira na mwenye sura iliyokuwa katika hali ya usiriazi zaidi.

“Go to hell”.Jamaa alijibu kama kumnong’oneza lakini sauti yake ikiwa yenye kiburi na wingi wa ujasiri.
Mkuu yule alionesha ghadhabu zake zahiri pale alipoepua birika lile lenye maji ya moto na kummwagia jamaa yule kifuani.

“Damn shit. You stupid.” Jamaa alitoa ukelele mmoja wa maumivu huku akirudi nyuma na kiti chake.

“Nakuuliza tena blood foolish,we ni nani na misheni yako ni nini”.Mkuu aliuliza kwa sauti ya juu huku bado hasira zake zikiwa kileleni.

“I was Born To die.Hata ufanye nini hupati kitu”.Jamaa alimjibu kwa sauti ya juu na ya maumivu kutoka mwilini mwake.
Mkuu kuona hivyo,akawaita wale wasaidizi wake na walikuja na kumkamata tena jamaa na kumvutia hadi pale mezani na mikono yake wakaiweka juu ya meza.

Mkuu wa sehemu ile akachukua uma kwenye kabati lililopo mle ndani na kisha akaanza kuirusha rusha na kuidaka huku akizunguka mle ndani huku na huko na maongezi yake yakiwa ya shari zaidi.

“Unajidai mgumu sana kijana.Leo tutaona.Na utakufa sababu ya ujinga wako”.Mkuu aliongea huku akimwelekea pale mezani na kumuuliza tena maswali yale yale.

“I was Born To Die”.Jamaa alijibu hivyohivyo kila alipoulizwa swali jambo lililompa hasira yule mkuu na kuwaambia wale wasaidizi wake waweke vizuri mkono wa kulia wa yule jamaa.

Alioona mkono umekaa sawia, alinyanyua juu ile uma aliyokuwa nayo na moja kwa moja akaituliza kwenye mkono wa jamaa.

“Aaaagh.You fuckin, your hurting me motherf**** (Aaagh.We mjinga unaniumiza (Akatukana)”.Jamaa alitoa kilio hicho kwa nguvu huku misuli yake ya shingo ikichomoza kwa sababu ya kujikaza wakati ile uma inaingia mkononi.

“Niambie wewe ni nani?”

“Nimekwambia sijui, nimezaliwa kufa”.Jamaa alijibu huku akilia kwa sauti ya juu.

“Mpigeni huyu.Mi nitarudi baada ya dakika kumi”.Mkuu aliwapa ruhusa wale wasaidizi na yeye akatoka nje.
Hapo hapo jamaa yule akaanza kupokea kipigo cha nguvu kutoka kwa wale jamaa watatu.

Waliompiga kichwani, walimpiga.Waliompiga mateke walimpiga, ili mradi walimpiga hadi akalegea na kushindwa hata kuongea.

Dakika kumi baadaye, mkuu alirudi na kumkuta jamaa kachakaa kwa damu na vimbe mbalimbali zikizidi kuongezeka katika mwili wake.

“Vizuri sana”.Aliwapongeza wale wasaidizi na kumfuata jamaa pale pembezoni mwa kona ya kile chumba alipokuwa amekaa.

“Sasa niambie.Wewe ni nani?” Swali lilelile liliulizwa.
Jamaa akamwangalia usoni na kutabasamu, tabasamu ambalo lililopotoka, lilitoka na michirizi ya damu mdomoni kwake.

“Unajisumbua tu!.I was Born To Die”Jamaa akajibu kwa sauti ya chini na kisha akamtemea mate yalichanganyikana na damu usoni kwa yule mkuu.

“Big mistake (Kosa kubwa)”.Mkuu alitamka na kutoa bastola yake kisha akampiga usoni kwa nguvu kwa kutumia kitako kile cha bastola.
Uso wa jamaa ukachanika lakini ndio kama alikuwa amempagawisha mkuu.Akampiga tena upande mwingine wa uso wake napo akapachana.Jamaa sasa akawa anavuja damu uso mzima zaidi ya mara ya kwanza.

“Tell me, who are you?(Niambie,wewe ni nani?)”.Mkuu aliuliza lakini hakupata jibu bali mihemo ya kasi kutoka kwa yule jamaa.

“I will kill you,blood foolish.(Nitakuua mpumbavu wewe)”.Mkuu alimuonya huku akiikoki bastola yake na kumwekea kichwani.

“I was Born To Die.I have nothing to loose (Nimezaliwa kufa, sina cha kupoteza)”.Jamaa alijibu kwa kulegea na taratibu akainamisha kichwa kwa ajili ya kuipokea ile risasi.

Mkuu naye akaanza kukibonyeza kile kifyatulio cha risasi huku akiwa makini asiifyatue hovyo huenda yule jamaa atasema chochote. Lakini hadi amefikia nusu ya ile triger, hakuna neno lililomtoka yule jamaa.Mkuu akafanya maamuzi yake ya mwisho.

-NI MAAMUZI GANI HAYO YA MKUU?
USIKOSE KESHO

Hakuna maoni:
Write maoni