RIWAYA: Born To Die
NA:Frank Masai
SEHEMU YA 1.
“What is your name? (Jina lako nani)?”
“I don’t know. (Sijui)”.
“Pu pu pu”.Zilisikika sauti hizo kwenye
chumba kimoja kidogo kilichokuwa na watu watano.
Sauti hizo zilikuwa ni sauti za kipigo
kumwendea yule aliyekuwa anaulizwa maswali.
Jamaa hao watano,mmoja ambaye ndiye
alionekana mkuu, alikuwa anauliza maswali,wengine wawili wamemshikilia kwa
nguvu jamaa mwingine aliyekuwa anaulizwa maswali,huku wamemkunja mikono kwa
nyuma na kufanya kifua na tumbo lake kubetuka vizuri kwa mbele.Kitu kilichompa
yule jamaa wa tano kumshushia kipigo cha nguvu pale alipokaidi kujibu maswali
yao.
“I asking you again.If you don’t answer, we
will kill you (Nakuuliza tena. Kama usipojibu, tunakuua)”.Yule mkuu wao ambaye
alivalia mavazi ya kijeshi, tena yale yenye nyota nyingi mabegani na kwenye
mifuko ya shati lake.Alimpa onyo jamaa yule aliyekuwa anapewa kipigo huku akiwa
amechakaa uso kwa damu pamoja na kuvimba vibaya mno.
Alishapoteza matumaini ya kuishi kwani
mwili wake ulikuwa umelegea kiasi kwamba alikuwa anawapa uzito wale waliokuwa
wamemshikilia.
“What is your name (Jina lako nani)?”Jamaa
aliulizwa swali.
“I don’t know Sir (Sijui Mzee)”.Alijibu
yule jamaa kwa sauti ya chini iliyokuwa imeishiwa nguvu kabisa.
Yule mpigaji alivyoona hivyo, alinyanyua
ngumi yake tayari kuendelea kuishindilia mwilini mwa yule jamaa.
“Stop (Acha)”.Yule mkuu alimkataza mpigaji.
“You are so rude, boy.That is good
(Unaonekana mkorofi kijana.Safi sana)”.Mkuu yule aliongea huku akizunguka
zunguka kile chumba kwa tambo.
“Release him.(Muachieni)”.Aliwaambia wale
jamaa waliokuwa wamemshika na wao wakatii amri kwa kumwachia yule mtuhumiwa
wao.
“You all, go outside (Ninyi nyote, nendeni
nje)”.Aliendelea kuwaamuru wale jamaa waliokuwamo mle ndani, nao wakatoka na
kumuacha yule jamaa kalala chini akigugumia kwa maumivu.
“Okey.Now we are alone.You have to tell me
the truth.(Sawa.Sasa tupo peke yetu.Unatakiwa kuniambia ukweli ”.Aliongea mkuu
yule huku akichutama karibu na pale alipokuwa amelala yule jamaa.
“I have nothing to tell you (Sina cha
kukuambia)”.Alijibu jamaa yule kwa sauti ya ukakamavu lakini iliyojaa maumivu.
“That’s bad boy. So damn bad. (Hiyo mbaya
kijana.Tena mbaya sana)”.Aliongea yule mkuu huku akisimama toka eneo lile na
kwenda kwenye jiko moja la umeme ambapo alikuwa ametenga birika la maji.
Akachukua birika lile na kwenda nalo kwenye
meza iliyokuwamo mle, kisha akamimina maji yale kwenye kikombe na kuchukua
kahawa kiasi kwenye kijiko na kuchanganya kwenye maji yaliyo kwenye kikombe.
Alivuta kiti kwa nyuma na kukikalia, kisha
akafunua sahani moja iliyokuwepo mezani pale na kuchukua chapati moja.
Aliikunja chapati ile na kuanza kuila huku
akishushia kwa kahawa aliyoichanganya muda mfupi uliopita.
Katikati ya ulaji wake, alimtupia jicho
yule jamaa aliyekuwa amelala pale chini.Alimwona jinsi anavyomwangalia alavyo, naye
akatumia udhaifu huo kuongea naye.
“Are you hungry? (Una njaa?)”.Alimuuliza
yule jamaa huku bado anatafuna kipande cha chapati alichokuwa kabwia mdomoni.
“Come on. Let’s eat. (Njoo. Njoo
tule)”Aliongea yule mkuu na kunyanyuka pale kitini na kwenda kwenye kabati moja
kuu-kuu la vyombo na kuchukua kikombe kimoja cha plastiki na kwenda nacho
mezani.
“Don’t you want it? (Hautaki?)”Alimuuliza
yule jamaa aliyekuwa amelala pale chini baada ya kumwona hajishughurishi
kuitikia karibu yake.
Jamaa yule aliyekuwa chini alianza kuinuka
pale alipokuwa na moja kwa moja akaelekea kuungana na yule mkuu kwenye meza
ile.
“That is my man.(Huyo ndiye mtu
wangu)”.Alimsifia jamaa alipokuwa ananyanyuka huku yeye akimimina maji kwenye
kile kikombe alichokuja nacho mara ya pili.
Jamaa naye alivuta kiti kiuchovu na kukaa huku
akimuelekea yule mwenyeji uso. Akapewa kahawa kwenye kikombe kile na kusogezewa
sahani ya chapati ili ajilie.
Alikula kwa taratibu na kistaarabu kuliko
alivyotegemea yule mkuu aliyekuwa anamuangalia kwa macho ya kumdadisi yule
jamaa ambaye alikuwa kifua wazi na chini kavaa kombati ya jeshi yenye mabaka ya
kijani.
“So.Tell me soldier boy. Who are you and
who sent you here (Niambie kijana. Wewe ni nani na nani kakutuma hapa?)”.Yule
mkuu alimuuliza huku akiweka miguu yake mezani.
“I am nobody and nobody sent me here. (Mi
si kitu na hakuna aliyenituma hapa)”.Jamaa alijibu na kisha aliinamia kahawa
yake na kuendelea kuinywa.
“You act like a taugh guy.Am I right boy? (Unajifanya
kijana mgumu sana.Nadanganya kijana?)”.Mkuu alimuuliza huku bado miguu yake
ikiwa pale mezani anaitikisa tikisa kwa mbwembwe.
“No. I just answer your questions. But if
you like me to be a tough guy,I will. But don’t blame me. (Hapana. Najibu
maswali yako. Lakini kama unapenda niwe mgumu, nitakuwa. Lakini
usinilaumu)”.Jamaa alijibu huku anasogeza kikombe cha kahawa na sahani mbele
kumuelekea yule mkuu.
“You never answer my questions boy. And
don’t try me to make you like before. (Hujanijibu maswali yangu kijana. Na
usinijaribu nikufanye kama hapo mwanzo)”.Mkuu aliongea huku macho yake kamkazia
yule jamaa ambaye alikuwa hataki kujitambulisha.
Jamaa alikaa kimya huku naye macho yake
anamuangalia yule mkuu ambaye umri kiasi fulani ulikuwa umeenda lakini alikuwa
bado mkakamavu.
Akiwa ndani ya mavazi yake ya nyota, mkuu
yule alishusha miguu yake juu ya meza na kusogea mbele zaidi na kumkingia uso
yule jamaa.
“Umetumwa na Urusi? Cuba au Korea?”Mkuu
yule alimuuliza kwa lugha ileile ya kiingereza.
Jamaa akacheka kwa dharau kisha akamuangalia
yule mkuu na kuhisi kama anapoteza dira.
“Kwa nini ziwe nchi hizo na siyo zile
mnazowatengenezea silaha za maangamizi na kuwapa ili muone kama zinafanya kazi
ipasavyo? Kwa nini zisiwe zile nchi ambazo mnazichukulia malighafi zake na
kujilimbikizia nyie? Kwa nini zisiwe zile nchi ambazo kila siku zinalia na njaa
huku zikipoteza watoto wake kwa waume kwa sababu ya vita ambavyo nyie ndio
wachonganishi? Kwa nini zisiwe nchi mnazozuga mnatandaza demokrasia, kumbe
mnatandaza vita? Kwa nini zisiwe hizi nchi mnazozitupia magonjwa kila kukicha?
Kwa
nini zisiwe nchi hizo na badala yake zikawa nchi ambazo zinatetea msifanye
maasi yenu?” Aliongea yule jamaa kwa sauti ya chini iliyoanza kupata ahueni
baada ya maumivu kupoa kiasi. Aliongea kwa hasira na msisitizo ndani yake.
“Kwa hiyo umetokea Afrika”.Aliongea yule
mkuu huku akirudisha mgongo wake kwenye kiti na kuweka miguu yake mezani tena
na mikono yake akiipitisha shingoni na kuja kukutana nyuma ya kisogo chake.
“Well, well.Umetoka Afrika. Niambie sasa.
Umetoka Kongo, Kameruni au Naijeria.Au labda umetoka Niger au Sudan”.Alizidi
kubwabwaja yule mkuu.
“Nimetokea Afrika.Siwakilishi nchi wala
Taifa”.Jamaa alijibu kwa nyodo na kwa kujiamini.
“Okey. Sasa ni muda wa kuwa siriazi. Nauliza
na unajibu ipasavyo, sawa?”Mkuu yule alikuja juu sasa na kumtaka yule jamaa
mwenye ngozi nyeusi awe siriazi.
“Ni wewe ndiye haupo siriazi. Nipo siriazi
hata kwenye kula.Ni vema uwahi kusema ulichokusudia kuliko kuniacha na kwa
kuendelea kuniuliza maswali. Sitataja jina langu,wala hutojua nipo hapa kwa
ajili gani”.Jamaa aliweka msisitizo kwa akifanyacho.
“Utakufa kijana”.Mkuu aliongea huku
akiendelea kumwangalia kwa uangalifu yule jamaa.
“I was BORN TO DIE”. Jamaa alimjibu mkuu na
kumuacha mkuu akiwa kinywa wazi bila kusema neno.
Maneno yale yalidhihirisha kuwa jamaa
haogopi wala kuhofia jambo lolote litakalokuja kumtokea mbeleni.
“Nakuuliza mara ya mwisho. Wewe ni nani na
nani kakutuma”.Mkuu aliuliza kwa hasira na mwenye sura iliyokuwa katika hali ya
usiriazi zaidi.
“Go to hell”.Jamaa alijibu kama
kumnong’oneza lakini sauti yake ikiwa yenye kiburi na wingi wa ujasiri.
Mkuu yule alionesha ghadhabu zake zahiri
pale alipoepua birika lile lenye maji ya moto na kummwagia jamaa yule kifuani.
“Damn shit. You stupid.” Jamaa alitoa
ukelele mmoja wa maumivu huku akirudi nyuma na kiti chake.
“Nakuuliza tena blood foolish,we ni nani na
misheni yako ni nini”.Mkuu aliuliza kwa sauti ya juu huku bado hasira zake
zikiwa kileleni.
“I was Born To die.Hata ufanye nini hupati
kitu”.Jamaa alimjibu kwa sauti ya juu na ya maumivu kutoka mwilini mwake.
Mkuu kuona hivyo,akawaita wale wasaidizi
wake na walikuja na kumkamata tena jamaa na kumvutia hadi pale mezani na mikono
yake wakaiweka juu ya meza.
Mkuu wa sehemu ile akachukua uma kwenye kabati
lililopo mle ndani na kisha akaanza kuirusha rusha na kuidaka huku akizunguka
mle ndani huku na huko na maongezi yake yakiwa ya shari zaidi.
“Unajidai mgumu sana kijana.Leo tutaona.Na
utakufa sababu ya ujinga wako”.Mkuu aliongea huku akimwelekea pale mezani na
kumuuliza tena maswali yale yale.
“I was Born To Die”.Jamaa alijibu hivyohivyo
kila alipoulizwa swali jambo lililompa hasira yule mkuu na kuwaambia wale
wasaidizi wake waweke vizuri mkono wa kulia wa yule jamaa.
Alioona mkono umekaa sawia, alinyanyua juu
ile uma aliyokuwa nayo na moja kwa moja akaituliza kwenye mkono wa jamaa.
“Aaaagh.You fuckin, your hurting me
motherf**** (Aaagh.We mjinga unaniumiza (Akatukana)”.Jamaa alitoa kilio hicho
kwa nguvu huku misuli yake ya shingo ikichomoza kwa sababu ya kujikaza wakati
ile uma inaingia mkononi.
“Niambie wewe ni nani?”
“Nimekwambia sijui, nimezaliwa kufa”.Jamaa
alijibu huku akilia kwa sauti ya juu.
“Mpigeni huyu.Mi nitarudi baada ya dakika
kumi”.Mkuu aliwapa ruhusa wale wasaidizi na yeye akatoka nje.
Hapo hapo jamaa yule akaanza kupokea kipigo
cha nguvu kutoka kwa wale jamaa watatu.
Waliompiga kichwani, walimpiga.Waliompiga
mateke walimpiga, ili mradi walimpiga hadi akalegea na kushindwa hata kuongea.
Dakika kumi baadaye, mkuu alirudi na
kumkuta jamaa kachakaa kwa damu na vimbe mbalimbali zikizidi kuongezeka katika
mwili wake.
“Vizuri sana”.Aliwapongeza wale wasaidizi
na kumfuata jamaa pale pembezoni mwa kona ya kile chumba alipokuwa amekaa.
“Sasa niambie.Wewe ni nani?” Swali lilelile
liliulizwa.
Jamaa akamwangalia usoni na kutabasamu,
tabasamu ambalo lililopotoka, lilitoka na michirizi ya damu mdomoni kwake.
“Unajisumbua tu!.I was Born To Die”Jamaa
akajibu kwa sauti ya chini na kisha akamtemea mate yalichanganyikana na damu
usoni kwa yule mkuu.
“Big mistake (Kosa kubwa)”.Mkuu alitamka na
kutoa bastola yake kisha akampiga usoni kwa nguvu kwa kutumia kitako kile cha
bastola.
Uso wa jamaa ukachanika lakini ndio kama
alikuwa amempagawisha mkuu.Akampiga tena upande mwingine wa uso wake napo
akapachana.Jamaa sasa akawa anavuja damu uso mzima zaidi ya mara ya kwanza.
“Tell me, who are you?(Niambie,wewe ni
nani?)”.Mkuu aliuliza lakini hakupata jibu bali mihemo ya kasi kutoka kwa yule
jamaa.
“I will kill you,blood foolish.(Nitakuua
mpumbavu wewe)”.Mkuu alimuonya huku akiikoki bastola yake na kumwekea kichwani.
“I was Born To Die.I have nothing to loose
(Nimezaliwa kufa, sina cha kupoteza)”.Jamaa alijibu kwa kulegea na taratibu
akainamisha kichwa kwa ajili ya kuipokea ile risasi.
Mkuu naye akaanza kukibonyeza kile
kifyatulio cha risasi huku akiwa makini asiifyatue hovyo huenda yule jamaa
atasema chochote. Lakini hadi amefikia nusu ya ile triger, hakuna neno
lililomtoka yule jamaa.Mkuu akafanya maamuzi yake ya mwisho.
-NI MAAMUZI GANI HAYO YA MKUU?
FUATANA NA MIMI KATIKA RIWAYA HII KILA SIKU, HAPAHAPA
Hakuna maoni:
Write maoni