Beyonce amechangisha dola 82,234 kwaajili ya kusaidia wakazi wa eneo la
Flint, Michigan nchini Marekani wanaokabiliwa na tatizo kubwa la maji.
Kwa mujibu wa Detroit Free Press, Queen Bey amekusanya kiasi hicho
cha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wakazi wa kitongoji cha Flint ambao
wameteseka kwa muda mrefu kutokana na mgogoro uliopo. Pia Beyonce
amewasaidia kuwalipia ada ya shule wanafunzi 14.
Queen Bey bado anaendelea na ziara yake ya ‘Formation’ huku June 28
akitarajiwa kufanya show kwenye jiji la Sunderland, Uingereza na Agosti 3
atakuwa nchini Hispania akiendelea na ziara yake kwenye jiji la
Barcelona.
Jumatano, 15 Juni 2016
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Write maoni