Rapper mkongwe na member wa kundi la Wateule, Solo Thang amesema kwa
sasa yupo mbioni kuanza kuandaa album yake mpya aliyoipa jina, S.U.M.U
ambayo ni kifupi cha ‘Sitaki Ujinga Maradhi na Umaskini.’
Akiongea na mtangazaji wa kituo cha redio cha Jembe FM, JJ, Solo alidai kuwa album hiyo inaweza kutoka mwakani.
“Ni big project ambayo naiandaa na inahitaji umakini mkubwa kwahiyo
sidhani kama itatoka mwaka huu inawezakana mpaka mwakani ndio ikatoka
kwasababu sasa hivi bado nipo kwenye maandalizi yake,” amesema.
Rapper huyo wa ‘Mambo ya Pwani’ amedai kuwa kwa sasa amerejea tena
shule kujiendeleza kielimu na anatarajia kuhitimu mwezi wa 10 na ndipo
ataanza rasmi kurekodi album hiyo.
Hivi karibuni alishirikisha na kwenye wimbo uitwao The Most wa rapper
wa Marekani Bolaji huku pia akishirikishwa na msanii wa Ireland, Neeve
na zingine.
Kwa sasa Solo amehamishia makazi yake nchini Ireland na amekuwa huko kwa miaka kadhaa sasa.
Jumatano, 15 Juni 2016
KIMYA KINGI KINA MSHINDO, Solo Thang kuja na album mpya iitwayo S.U.M.U
Similar Posts
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Write maoni