Jumatano, 1 Juni 2016

HUYU NDIYE STAA MPYA WA FILAMU ZA JAMES BOND - 007?

 

 

Tom Hiddleston

 

Alizaliwa Tarehe 9 Februari, 1981 na muigizaji wa Kiingereza. Kacheza Filamu kama LOKI, THOR ya mwaka 2011, THOR: The Dark World ya 2013, The Avengers, The War Horse na nyingine nyingi.

Mabosi wa James Bond au 007 kwa jina lake la 'tata', wamemuangalia nyota huyu wa Kiingereza kuwa James Bond anayefuata baada ya Daniel Craig kumaliza muda wake.

Barbara Broccoli ambaye ndiye 'Boss' mkuu wa James Bond, ameweka bayana kumtilia jicho Staa huyu ambaye alipata umaarufu zaidi kwenye filamu yake ya Thor ambayo alikuwa anacheza na rungu ambalo hamna anayeweza kulinyanyua zaidi yake.

Japokuwa mweusi mwingine, Idris Elba naye alitazamwa, lakini yaonekana Boss mkuu ameangalia pia vigezo kwa sababu Tom ndiye Kipenzi kipya cha wapenda 'Movies' hasa baada ya bwana huyu kuonekana kwenye kipindi cha runinga au 'Series' ya Kipelelezi iitwayo The Night Manager inayorushwa kwenye kituo cha BRITISH TV.

Tom pia yupo katika watu wanaotazamiwa kwenye filamu ya Fast And Furious 8 itakayotoka mwakani mwezi wa nne. Muongozaji wa filamu hii aliweka bayana kuwa anahitaji muigizaji wa Kiingereza awepo kwenye 'scenes' zake, na jicho la kwanza lilimuangalia,  Tom Hiddleston.

Na zaidi, The Rock atakuwepo kwenye filamu ya Fast And Furios 8.

Hakuna maoni:
Write maoni