Rapa Fid Q aliwahi kusema “Ustaa ni mzigo wa mwiba ukiubeba lazima
utaumia” well hii sio siri kwa watu wengi maarufu ambao waliwahi
kutamani kuishi kistaa na sasa wanajutia hali hio.
WCB staa Harmonize naye ameanza kujutia maisha ya ustaa kupitia ujumbe
wake instagram kuhusu mategemeo ya maisha ya umaarufu ni tofauti na
alivyowazia.
Harmonize aliandika hivi
“Nilikuwa
Sijuwi Kuwa Umaarufu Una Mambo Mengi Kiasi Hikii Daaah Sio Rahisi
Kuyashinda Peke Yangu M/mungu Simama Nami Hadi Siku Yangu Ya Mwisho
Umaarufu Isiwe Sababu Ya Kukukosea Na Kuwakosea Wazazi Wangu Pamoja Na
Ndugu Rafiki Pia Nakuomba Unijalie Mwisho Mwema Mimi Na Nduguzangu
Woooote Walio Bahatika Kusoma Hapa Tuseme Ameen 

”



Hakuna maoni:
Write maoni