Jumamosi, 18 Juni 2016

Olimpiki: Jiji la Rio lakabiliwa na uhaba wa fedha



Gavana wa Jiji la Rio de Janeiro amesema kuwa jimbo lake limeishiwa na fedha za kutoa huduma za umma - siku hamsini tu kabla ya kuanza michezo ya Olimpiki.
Francisco Doernelles amesema kwamba amelazimika kutangaza hali ya hatari ya kifedha ili kuomba Serikali Kuu ya Brazil kusaidia katika juhudi za kuandaa michezo hiyo.

Alisema hali ya kifedha ya sasa inaweza kuzuia Rio kutekeleza majukumu yake katika michezo ya Olimpiki ya walemavu.
Hatua madhubuti zinatekelezwa katika utoaji huduma wa usalama, uchukuzi na huduma zingine za umma.

Alisema bila msaada wa aina hiyo shughuli zote za uandaaji wa michezo hiyo zitaporomoka.

Rais Michel Temer, aliyetembelea Rio juma hili alisema kuwa atahakikisha kuwa huduma zote zinazohitajika zinatekelezwa.

Hakuna maoni:
Write maoni