Jumamosi, 18 Juni 2016

Fallujah Yakombolewa kutoka kwa IS

 
 
 
Waziri mkuu wa Iraqi, Haider al Abadi, ametangaza kuwa mji wa Faluja umekombolewa na wanajeshi wa Serikali.

Katika taarifa fupi aliyoitoa kwa runinga ya kitaifa moja kwa moja, bwana Abadi alisema kuwa makundi machache ya wapiganaji wa Kiislamu wenye itakadi kali wa Islamic State wangali Falujjah, lakini akawahakikishia wananchi kuwa watatimuliwa baada ya muda mfupi.

Bwana Abadi, aliyekuwa ameandamana na maafisa wa vyeo vya juu jeshini, alisema kuwa mji wa Kaskazini wa Mosul, ambao ni ngome kuu ya Isis, ndio unaolengwa sasa na wanajeshi wake.

Mapema, wanajeshi wa Iraq walikomboa mijengo ya Serikali jijini Fallujah na kupandisha bendera katika uwanja wa Serikali.


Walifanya hivyo majuma manne baada ya mapigano kuanza.

Fallujah, ambao ni mji ulio kilomita 50 Magharibi mwa Badghdad, umeshikiliwa na IS kwa muda mrefu kuliko miji mingine nchini Syria.

Hakuna maoni:
Write maoni