Rich Mavoko, Ommy Dimpoz, Cpwaa, Q-Chief, Chege na Temba ni miongoni mwa
wasanii waliowahi kusafiri na muongozaji wa video, Adam Juma kwenda
kufanya video zao Afrika Kusini.
Na sasa huenda ndoto ya wasanii wengine wenye nia ya kukwea pia na AJ
ili kufanya video zao bondeni huenda zikawa zimefutika rasmi. Ni
kwasababu muongozaji huyo amesema kwa sasa (walau kwa sasa) hana mpango
tena wa kwenda kufanya video zake nchini humo.
“Yaani sasa hivi mtu akiniambia anataka kwenda kushoot video South
Africa siendi tena,” Adam alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM
ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka.
“Siwezi kwenda, sasa hivi nina commitment, watoto wanataka kwenda
shule. Unalipwa hela ile ile kazi ambayo unaifanya hapa kwa siku moja,
it doesn’t make any sense,” aliongeza.
“Mimi nimefanya video nyingi South Africa, lakini nimefanya kwasababu
ya kuinvest, lakini sasa ukija kuangalia kwa faida kitu gani tunapata?”
AJ ameendelea kusisitiza kuwa uongozaji wa video kwa Tanzania bado
haulipi na hiyo ni sababu iliyomfanya aache kufanya kazi nyingi kama
zamani. Amesema kwa sasa atafanya kazi na wasanii ambao wako tayari
kumlipa vile anavyotaka au mahitaji muhimu yanayohitajika kufanikisha
wazo la video husika.
Hivi karibuni waongozaji wengine wa video nchini wameanzisha
utaratibu wa kwenda na wasanii kufanya video Afrika Kusini. Mfano ni
video ya Chafu Pozi ya
Bill Nass na Pesa ya Madafu ya Jay Moe ambazo
zote zilifanyika SA na kuongozwa na Msafiri wa Kwetu Studios.
Waongozaji wanadai kuwa sababu kubwa inayowapeleka Afrika Kusini
kufanya video ni upatikanaji rahisi wa location ambapo kwa Tanzania
huwawia vigumu kutokana na kutokuwepo utaratibu maalum na huku mamlaka
zingine zikiwa na mchakato mrefu wa kuruhusu kutumiwa kwa maeneo husika.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Write maoni