Jumatano, 15 Juni 2016

HAWA NDIO WATAONESHA KAZI JUKWAANI KWENYE BET YA JUNE 26

Future, Usher, na Bryson Tiller wametangazwa kuongezwa kwenye orodha ya wasanii watakaotumbuiza siku hiyo. Wanaungana na mastaa wengine waliokuwa wametangazwa awali ambao ni pamoja na Alicia Keys, Maxwell, pamoja na tribute ya Prince itakayotolewa na D’Angelo, The Roots na Janelle MonĂ¡e.

Mastaa watakaokabidhi tuzo ni pamoja na DJ Khaled, Gabrielle Union, Tinashe, Fantasia, Regina Hall, Birdman, Jermaine Dupri, Dame Dash na Snoop Dogg.
Diamond ni miongoni mwa wasanii wanaowania tuzo hizo mwaka huu kwenye kipengele cha Best International Act: Africa.

Washereheshaji wa show hiyo watakuwa ni Anthony Anderson na Tracee Ellis Ross.
Tuzo hizo zitatolewa June 26 live kutoka Microsoft Theater, Los Angeles, Marekani.

ENDELEA KUMPIGIA KURA DIAMOND PLATNUM ILI ARUDI NA TUZO HIYO.

Hakuna maoni:
Write maoni