Kwa mujibu wa kundi la madkatari wasio na mpaka MSF raia wanaendelea
kuathirika na ghasia katika mji wa Taiz nchini Yemen, licha ya sitisho
la mapigano ambalo lilifikiwa miezi miwili iliyopita baina ya pande
zinazozozana.
Baadhi ya mapigano makali na upigaji makombora umefanyika katika
maeneo yenye wakazi wengi ya Taiz, huku makombora ya kila siku,
mashambulizi ya anga, milipuko ya mabomu, milipuko ya mabomu ya kutegwa
ardhini na mashambulizi ya walenga shabaha, kundi hilo la misaada ya
kiafya limesema jana na kuongezea kuwa mapigano na upigaji makombora
unafanyika katika maeneo yenye raia wengi mjini humo.
Hakuna upande unaozozana unaonekana kufanya juhudi za kujuia majeruhi miongoni mwa raia, taarifa hiyo ilisema.
MSF imezitaka pande zote katika mzozo wayemen huo kuchukuwa hatua
kubwa kuwalinda raia, kupunguza kiwango cha mzozo na kufungua njia ya
kufanikisha upelekaji misaada ya kibinadam huko Taiz.
Mjumbe maalum wa umoja mataifa kwa yemen, Ismail Ould Cheik Ahmad
alikutana katika muundo wa mashauriano ya amani na wapatanishi
waandamizi wa yemen wanaoshiriki katika mazungumzo ya amani ya Yemen
nchini Kuwait.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Write maoni