Jumanne, 7 Juni 2016

RAIS MAGUFULI AMTEUA KUWA JAJI KIONGOZI,JAJI FERDINAND LEONS KATIPWA WAMBALI



Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Jaji Kiongozi na kumteua Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuchukua nafasi hiyo.
Katika taarifa ambayo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msingwa na kueleza kuwa nafasi hiyo imechukuliwa na Jaji Ferdinand baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Jaji Shaaban Ally Lila ambaye alibadilishiwa kazi na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Jaji Ferdinand kabla ya kuteuliwa kuchukua nafasi hiyo alikuwa ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Tanga.
WhatsApp-Image-20160607

Hakuna maoni:
Write maoni