Jumapili, 29 Mei 2016

RAIS WA REAL MADRID ALIONGEA HAYA BAADA YA KUNYANYUA NDOO.

"Najisikia fahari sana ndani ya Real Madrid, ya mashabiki, wachezaji na historia yake.", Alisema rais.

Rais wa Real Madrid, Florentino Pérez, alizungumza na vyombo vya habari kufuatia timu hiyo kutwaa ubingwa huko San Siro: 

"Najisikia fahari sana juu ya Real Madrid, ya mashabiki, wachezaji na historia yake. Napenda kujitolea maneno machache kwa Atlético Madrid kwa sababu walifanya juhudi kubwa ". 

Pia akamzungumzia Kocha aliyeichukua Real Madrid baada ya Carl, namzungumzia Zinedine Zidane.

  "Zidane amekuwa muhimu sana. Ameibadilisha historia, ameshinda kombe hili kama mchezaji na kocha, sawa na mimi kama mchezaji, nlifanya hivyo, rais". 

"Kwa hisia, napenda kupeleka ushindi huu kwa washabiki wetu wa nchini Iraq, waliyoonesha thamani ya kuwa mashabiki wa Real Madrid.

 Shindano muhimu zaidi

 "Kila msimu ni mgumu. Katika La Liga tulikuwa tupo mbali kipoint, ni vigumu daima. Tumepigana na tulikuwa na msimu mzuri. 
 Ligi ya Mabingwa ni DNA yetu, ni muhimu zaidi na tunathamini kuliko kitu kingine chochote duniani."  

Sergio Ramos

 "Napenda binafsi kumshukuru Sergio Ramos kwa ajili ya msimu wake mkubwa. Katika Januari alichukua uzito wa timu juu ya mabega yake. Kila mtu anajua kwamba nataka akae kwa sababu yeye ni sehemu muhimu ya historia yetu ".

 Uchovu

 "Kulikuwa na mengi ya matukio ya msuli, lakini ni jambo la kawaida. Wao hawakuwa na la kushikilia huko nyuma. Katika Desemba tumechambuwa kila hali na tulikuwa na mengi ya imani na Zidane. 

Sisi daima hucheza vizuri katika fainali ".

Hakuna maoni:
Write maoni