Jumamosi, 18 Juni 2016

MICROSOFT NAYO YAANZA KUUZA BANGI




Kampuni ya Microsoft imekuwa ya hivi karibuni kujiunga na biashara ya kuuza bangi katika majimbo ya nchini Marekani ambako inaruhusiwa kwa mujibu wa sheria za majimbo hayo.

Kampuni hiyo imeungana na kampuni nyingine "Kind Financial - inayotengeneza programu za kusaidia wadhibiti kufuatilia uzalishaji na mauzo ya bangi.

Majimbo kadhaa nchini Marekani yameruhusu uuzaji wa bangi kwa matumizi ya kimatibabu na kujistarehesha, japo imeharamishwa chini ya sheria kuu za nchi hiyo.

Hakuna maoni:
Write maoni