Hivi karibuni kumeibuka taarifa kuwa ule ukaribu uliokuwepo mwanzo kati
ya kundi la Navy Kenzo na Weusi umepotea tangu yalipofanyika mabadiliko
ya studio ya The Industry. Nahreel amesema hilo siyo kweli bado ni
washkaji kama zamani tofauti watu wanavyowachukulia.
Navy Kenzo na Weusi wamekuwa watu wa karibu sana hali iliyopelekea
watu kuona wivu kwa kusema kuwa Nahreel anawapendelea wasanii hao kwa
kuwatengenezea beat nzuri zaidi ya wasanii wengine.
Akiongea na Bongo5, Nahreel amesema kuwa wao na Weusi bado ni washkaji na bado wana kazi zao kwenye studio yake hazijatoka.
“Ni kweli utaratibu umebadilika na mimi kama mfanyabiashara mwingine
lazima kila siku niendelee kuweka utaratibu fulani,” alisema Nahreel.
“Hapa kati nimekuwa busy na ratiba zangu na focus na Navy Kenzo
tumekuwa tuna move hapa na pale kwahiyo unajua Weusi na wao wana mipango
yao kama wana muziki siwezi nikawa mimi tu nawacheleweshea time zao,
na hapa wana nyimbo nyingi zipo bado hazijatoka,” aliongeza.
Hata hivyo Mei 6 mwaka huu Navy Kenzo walifanya sherehe za kuzindua
studio yao ‘The Industry lakini hakuna hata msanii mmoja wa kundi la
Weusi aliyehudhuria sherehe hizo.
Jumamosi, 18 Juni 2016
Nahreel, hana tatizo na Weusi
Similar Posts
Next
Prev Post
Prev Post
About Unknown
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Write maoni